1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Guterres: Uvamizi wa Urusi umekiuka sheria za kimataifa

25 Oktoba 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemueleza Rais Vladimir Putin wa Urusi kwamba uvamizi wake nchini Ukraine ulikiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

https://p.dw.com/p/4mCxK
Kazan Urusi 2024 | Vladimir Putin akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akipeana mkono na Rais Vladimir Putin kwenye mkutano wa kilele wa kundi la BRICSPicha: Alexander Nemenov/AFP

Guterres alikutana na Putin pembezoni mwa mkutano wa kilele wa kundi la BRICS huko Kazan, Urusi, baada ya hotuba yake iliyotoa wito wa "amani ya haki" nchini Ukraine.

Guterres pia alisisitiza dhamira yake ya "kuanzisha urambazaji huru katika Bahari Nyeusi," akisema hatua hiyo ni muhimu kwa Ukraine, Urusi, pamoja na "usalama wa chakula na nishati duniani."

Bahari Nyeusi ni njia muhimu ya biashara ya Ukraine, moja ya wauzaji wakubwa wa nafaka ulimwenguni, lakini imekumbwa na vizingiti tangu kuanza kwa vita hivyo mapema, 2022.