Guterres aonya juu ya kuboreshwa kwa silaha za nyuklia
30 Agosti 2023Matangazo
Katika taarifa ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na majaribio ya nyuklia, Guterres amesema kwamba kuna silaha za nyuklia zipatazo 13,000 duniani kote, na kueleza umuhimu wa kupiga marufuku majaribio ya nyuklia kuelekea ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia.
Mkataba wa kupiga marufuku majaribio ya nyuklia una nchi wanachama 196 huku 186 kati yao wakiutia saini na 178 kuuidhinisha, zikiwemo nchi nane katika muda wa miezi 18 iliyopita.
Katika mkutano wa kuadhimisha siku hiyo, hapakuwa na dalili kuwa nchi hizo nane - Marekani, China, Misri, Israel, Korea Kaskazini, India na Pakistan - zinaelekea kuutekeleza mkataba huo.
Umoja wa Mataifa ulitangaza Agosti 29 kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Majaribio ya Nyuklia.