Guterres atahadharisha dhidi ya kuishambulia Rafah
26 Februari 2024Matangazo
Akilihutubia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Guterres alisema kuwa mji huo wa Rafah unaopakana na Misri na ambako zaidi ya Wapalestina milioni 1.4 wamekimbilia kusaka hifadhi, ndio kiini cha operesheni ya misaada ya kibinaadamu katika Ukanda wote wa Gaza.
Soma zaidi: Juhudi mpya zaanzishwa ili kusitisha mapigano Gaza
Matamshi yake yanakuja baada ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kusisitiza kwamba nchi yake ina nia ya kuivamia Rafah katika jitihada zake za kutafuta ushindi kamili dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas.