1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Guterres atoa heshima kwa wafanyakazi wa UN waliouawa Gaza

24 Desemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa heshima zake kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliouawa katika vita kwenye ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4aWRo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa - Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York mnamo Desemba 8, 2023
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa - Antonio GuterresPicha: YUKI IWAMURA/AFP

Katika ujumbe alioandika katika mtandao wa kijamii wa X ambao awali ulijulikana kama twitter, Guterres amesema kuwa wafanyakazi 136 wa Umoja wa Mataifa wameuawa katika ukanda huo ndani ya siku 75, na kwamba wengi wa wafanyakazi hao wamelazimishwa kutoka majumbani mwao.

Soma pia: Zaidi ya Wapalestina 20,000 waelezwa kuuwawa Gaza

Guterres ameendelea kusema kwamba "anatoa heshima zake kwa maelfu ya wafanyikazi wa misaada wanaohatarisha maisha yao kuwasaidia raia katika eneo hilo la mapigano.

Katika chapisho jingine, Guterres kwa mara nyingine alikosoa hatua za Israel katika mzozo huo na kusema  jinsi Israeli inavyoendesha mashambulizi hayo, inasababisha vikwazo vikubwa kwa usambazaji wa misaada ya kibinadamu ndani ya Gaza.

Soma pia:UN yahimiza msaada zaidi Gaza baada ya kupitishwa azimio

Guterres ameongeza kuwa ili kufanikiwa kufikisha misaada ya kibinadamu Gaza, usalama na wafanyakazi wanaoweza kufanya kazi kwa usalama wanahitajika.