1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMorocco

Guterres na mfalme wa Moroko wajadili Sahara Magharibi

24 Novemba 2022

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya mkutano wa nadra na Mfalme Mohammed wa Sita wa Moroko jana Jumatano, na kujadili eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

https://p.dw.com/p/4JzQa
Wahlen in Marokko | König Mohammed VI.
Picha: Azzouz Boukallouch/DNphotography/abaca/picture alliance

Kulingana na taarifa kutoka falme hiyo, Mfalme Mohammed alisisitiza msimamo wa Moroko kwamba mzozo wa eneo hilo unapaswa kusuluhishwa ndani ya mfumo wa uhuru na mamlaka na mipaka ya falme hiyo.

Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba Guterres na mfalme wamejadili hali katika kanda na, hasa katika Sahara Magharibi.

Moroko inachukulia Sahara Magharibi kama "mikoa yake ya kusini" , eneo ambalo ilidhibiti kabla ya kunyakuliwa na mkoloni Uhispania.