Guterres: Raia wa Gaza wanakabiliwa na hali 'mbaya sana'
10 Oktoba 2023Guterres amesema amefadhaishwa na tangazo la Israel kuwa ingeweka mzingiro kamili dhidi ya ukanda wa Gaza, ikizuia kikamilifu kuingizwa kwa chakula, maji na nishati ya umeme.
Soma pia:Mzozo kati ya Israel na Hamas wazidi kutokota
Katibu Mkuu Guterres amesema anatambua uhalali wa wasiwasi wa Israel kuhusu usalama wake.
Scholz asema vita baina ya Israel na Hamas havipaswi kuchochewa zaidi
Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, amesema vita baina ya Israel na Hamas havipaswi kuchochea zaidi moto wa uhasama, na kuongeza kuwa ugaidi hautashinda. Akiwa pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Hamburg, viongozi hao wawili wamesema wanasimama pamoja na Israel.
Soma pia:Serikali ya Israel yawaamuru wanajeshi wake kulizingira eneo la Ukanda wa Gaza
Hayo yakiarifiwa, Umoja wa Ulaya umefuta kauli yake ya awali kuwa unasitisha msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina. Aidha, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameutaka upinzani nchini mwake kuridhia kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa bila masharti yoyote, wakati nchi hiyo ikiendelea na operesheni za kulipa kisasi dhidi ya Hamas.