1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakainde Hichilema ashinda uchaguzi wa rais Zambia

Daniel Gakuba
16 Agosti 2021

Hakainde Hichilema ametangazwa mshindi katika kinyang'anyiro cha urais Zambia, akimuangusha rais wa sasa Edgar Lungu.

https://p.dw.com/p/3z1tG
Sambia Hakainde Hichilema
Picha: Getty Images/AFP/D. Salim

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zambia imemtangaza Hakainde Hichilema kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika Alhamis iliyopita, akimbwaga rais wa sasa Edgar Lungu.

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ya Zambia Esau Chulu ameyatangaza matokeo rasmi asubuhi ya leo Jumatatu, baada ya kupatikana hesabu za majimbo yote isipokuwa moja tu. Hesabu hizo zimeonyesha kuwa Hakainde Hichilema wa chama cha United Party for National Development (UPND) amepata kura 2,810,777 akimpita kwa mbali rais wa sasa Edgar Lungu kutoka chama cha Patriotic Front (PF) aliyepata kura 1,814,201.

Wapiga kura milioni 7 walikuwa wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye idadi jumla ya wakaazi karibu milioni 19. Hapo jana Rais Lungu alikuwa amesema uchaguzi huo haukuendeshwa katika mazingira huru na haki, na kutishia kukataa matokeo yake. Hii ilikuwa mara ya sita kwa Hakainde Hichilema kugombea wadhifa huo.

Taarifa zaidi inafuata punde...