1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya Trump na Kim

Yusra Buwayhid
28 Februari 2019

Rais Donald Trump wa Marekani amesema alitoka mkutanoni na kumuacha Kim Jong Un wa Korea Kaskazini, kwasababu kiongozi huyo alitaka vikwazo vyote ilivyowekewa nchi yake viondolewe.

https://p.dw.com/p/3EERn
Vietnam l Trump nach Gipfeltreffen mit  Kim Jong Un in Hanoi
Picha: Reuters/J. Silva

Rais wa Marekani Donald Trump amesema leo kwamba alitoka kwenye mkutano wa kilele kuhusu makubaliano ya mpango wa nyuklia na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un kwasababu ya masharti yasiyowezekana ya kiongozi hiyo ya kutaka nchi yake iondolewe vikwazo ilivyowekewa kwa uchochezi wa Marekani.

Mapema, viongozi wote wawili, Trump na Kim walikuwa na matumaini ya kupatikana maendeleo katika kuboresha uhusiano wao kuhusu suala muhimu la silaha za kinyuklia, wakati wa mkutano wao wa pili wa kilele katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi, ikiwa ni miezi minane baada ya mkutano wao wa kwanza wa nchini Singapore.

"Ilikuwa ni kuhusu vikwazo tu," alisema Trump katika mkutano na waandishi habari baada ya mkutano wake na Kim kuwa mfupi kuliko ilivyotarajiwa. "Kimsingi walitaka vikwazo walivyowekewa viondolewe kiukamilifu, hatuwezi kufanya hivyo."

Marekani na Umoja wa Mataifa kwa pamoja waliiwekea vikwazo Korea Kaskazini, baada ya taifa hilo kufanya mfululizo wa majaribio ya makombora ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu mwaka 2017.