1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya biashara ya binadamu nchini Ujerumani.

Sekione Kitojo15 Julai 2009

Watu kufanyishwa kazi kwa nguvu , pamoja na utumwa wa kimamboleo ni hali inayowakumba wahamiaji haramu katika nchi za magharibi, na hata hapa nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/IqJc

Watu kufanyishwa kazi kwa nguvuu, na utumwa ni maneno ambayo baadhi ya Wajerumani kwa kweli huwakumbusha nyakati za usoshalist wa kizalendo, ama biashara ya utumwa katika historia ya kale ya Marekani.

Lakini, hata hii leo kuna mfumo wa kimamboleo wa watu kulazimishwa kufanya kazi na utumwa, hata hapa Ujerumani. Jambo la ajabu ambalo hutokea katika baadhi tu ya hali na dhahiri kabisa huwa ni vigumu kulielewa. Wahanga wanaendelea kubaki gizani, wakati mara zote wakiendelea kuishi hapa nchini Ujerumani kinyume na sheria. Watu hawa wanapaswa kupewa sauti na mashirika yanayoshughulika haki za binadamu na kuwasaidia kuweza kudai haki zao.



Wanafanya kazi za kushughulikia chakula, katika majumba wa watu binafsi, ama kama wafanyakazi wa biashara ya ngono katika madanguro. Ni wangapi watu hawa, hakuna mtu anayefahamu vizuri.

Ndio sababu, wengi wanaishi bila kuwa na hati za kuishi hapa Ujerumani, na wana wasi wasi wa kurejeshwa makwao.

Hakuna mtu anayeweza kusema kwa dhati, iwapo watu wanaolazimishwa kufanya kazi na biashara ya watu hapa nchini Ujerumani ni tatizo la mipaka ama ni tatizo la kuingia watu wengi. Kwamba kuna mfumo wa kisasa wa utumwa, hilo halina shaka kabisa. Ushahidi unapatikana katika kile kinachoelezwa kuwa ni ripoti ya hali ya watu kama hao katika idara ya uhalifu ya Ujerumani.

Pekee katika mwaka 2007, chini ya kichwa cha habari, utumiaji watu katika ngono, uchunguzi umefanyika katika matukio 450 , kutokana na matukio 700 yaliyoorodheshwa.

Wahanga wa kusaidiwa, ni lengo lililoelezwa katika miradi ya taasisi ya Ujerumani inayohusu haki za binadamu na wakfu wao wa ukumbusho, wajibu na hali ya baadaye, kiongozi wake, Martin Salm, ameonyesha matumaini makubwa ya hapo baadae.

Ni ishara kwa wote wanaohusika kuwa wana haki na kuna nafasi ya kupatiwa usaidizi. Ni ishara kwa jamii yote, kwa jumla, kuwa kuna watu wanaolazimishwa kufanya kazi nchini Ujerumani, na haiwezekani kuwepo hali ya kuvumilia kuhusiana na utumwa mambo leo na watu kulazimishwa kufanyakazi. Na ni ishara kwa wale wanaofanya hivyo. Wanaweza kukamatwa na inaweza kuwagharimu kwa kiasi kikubwa. Inaweza kuwa sheria ikachukua mkondo wake, inaweza kuwa pia ni kulipa fidia dhidi ya mshtakiwa.



Kwa mtazamo wa kwanza, inaonyesha kuwa kwa muda wa miaka mitatu ya kutokuwa na fedha za kutosha, pamoja na usaidizi unaofikia kiasi cha Euro 600,000, katika mradi huo unaonyesha kupata mafanikio madogo.

Wasi wasi wa kuamini maeneo ya kutoa ushauri ama watendaji kuweza kushtakiwa, ni mkubwa. Utendaji wa mahakama za Ujerumani unaonyesha wasi wasi wa kutoa haki. Na tena baadhi ya wahanga wanakuwa mashahidi, wakati madai yao ya fidia hayaangaliwi, amekosoa mkurugenzi wa taasisi ya Ujerumani ya haki za binadamu, Heiner Bielefeldt. Anaeleza hususan kwamba masuala ya haki za binadamu hayagawanyiki na yako mbele kabisa. Haki za binadamu zina nafasi kubwa kuliko hati ya kuishi nchini.

Pia watu ambao wanajikuta katika hali ya kuishi bila vibali, na ambao huenda pia wamevunja sheria na kusafirishwa kwa kibiashara, pia wana haki za binadamu. Haki ya kibinadamu haihusiani na hadhi aliyonayo mtu, kisheria, katika nchi, pia sio katika uhalali wa viza ya kuishi nchini .


Anayoyasema Bielefeldt hata serikali ya Ujerumani ndio inayoyaamini. Kwa wito wa mkurugenzi wa taasisi hiyo, makubaliano yaliyokwisha fikiwa 2005 yanatarajiwa kuidhinishwa na bunge la Ulaya dhidi ya usafirishaji wa watu.


Mwandishi Sekione Kitojo/ZR

Mhariri Othman Miraj.

►◄