1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya hatari yatangazwa kwenye jimbo la Belgorod

14 Agosti 2024

Maelfu ya watu wamehamishwa baada ya mashambulio ya majeshi ya Ukraine kwenye majimbo ya mpakani ya Belgorod na Kursk katika ardhi ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4jRfV
Urusi Belgorod | mgogoro wa Urusi na Ukraine
Hali ya hatari yatangazwa kwenye jimbo la BelgorodPicha: Yevgeny Martynov/ITAR-TASS/IMAGO

Gavana wa jimbo la Belgorod amesema hali ni ngumu kwa wakaazi wa sehemu hizo.

Wakati huo huo rais wa Marekani Joe Biden amesema rais Putin yupo njia panda baada ya majeshi ya Ukraine kudhibiti eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 40 ndani ya jimbo la Kursk.

Urusi, Ukraine mambo yazidi kuwa mabaya

Mkuu wa majeshi wa Ukraine Oleksandr Syrsky, ameeleza kuwa majeshi yake yanadhibiti eneo hilo tangu siku ya Jumanne.

Naye gavana wa mkoa wa Kursk, Alexei Smirnov, amesema makazi 28 yalitekwa na vikosi vya Ukraine siku ya Jumatatu yalipopenya takriban kilomita 12 ndani ya ardhi ya Urusi.