1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yakataa matakwa mapya ya Israel usitishaji vita Gaza

26 Agosti 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas limesema limeyakataa masharti mapya ya Israel kuhusu mazungumzo ya usitishaji mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4jvDr
Ukanda wa Gaza| Mashariki ya Kati
Hali kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Abood Abusalama/Middle East Images/IMAGO

Tangazo hilo la Hamas linazidisha mashaka juu ya mustakabali wa kupatikana mwafaka katika juhudi za karibuni zinazoungwa mkono na Marekani za kumaliza vita vya miezi kumi.

Hata hivyo, mshauri wa usalama wa taifa wa Ikulu ya White House Jake Sullivan, amesema kwamba Marekani bado inahangaikia kufikiwa kwa makubaliano hayo, licha ya mashambulizi ya Jumamosi kati ya Hezbollah na Israel.

"Ninachoweza kukuambia ni kwamba bado tuna mawasiliano endelevu na wenzetu wa Israel katika ngazi zote. Na wametushirikisha jinsi wanavyoona hali nasi tumewashirikisha namna tunavyoiona hali na tulijaribu kuratibu kwa ukaribu kadri iwezekanavyo." amesema Sullivan.

Wakati huo huo, idadi ya vifo vya Wapalestina vilivyotokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza sasa imefikia 40,405, kulingana na mamlaka ya afya ya Gaza.