Hamas yamtangaza Yahya Sinwar kuwa kiongozi mpya
7 Agosti 2024Kundi la wanamgambo la Hamas limemtangaza Yahya Sinwar kuwa kiongozi wake mpya. Tangazo hilo linafuatia kifo cha kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyehaliyeuawa mjini Tehran wiki iliyopita.
Sinwar, kiongozi wa juu wa kundi la wapiganaji wa Kipalestina huko Gaza, anaaminika kuwa ndiye aliyepanga mashambulizi ya kigaidi ya Oktoba 7 dhidi ya Israel ambayo yalisababisha takriban watu 1,200 kuuawa.
Kundi la Hamas pia liliwachukua mamia ya mateka kutoka Israel, ingawa karibu nusu waliachiliwa wakati wa makubaliano ya Novemba. Israel, Marekani na Umoja wa Ulaya zinalitambua Hamas kuwa kundi la kigaidi.
Wakati huo huo, viongozi wa kikanda na ulimwengu wanaendeleza juhudi za kuepusha mzozo zaidi Mashariki ya Kati. Iran, Hezbollah na makundi mengine yameapa kulipiza kisasi baada ya shambulio la Israelkumuua kamanda wa juu wa Hezbollah huko Beirut.