1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hamas yawaachia mateka wawili iliokuwa ikiwashikilia

21 Oktoba 2023

Israel imethibitisha kuwa Hamas imewaachia huru mateka wawili iliokuwa inawashikilia, na tayari wamekabidhiwa kwa jeshi la Israel kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4Xq7l
Judith und Natalie Raanan | amerikanisch-israelische Staatsbürgerinnen
Picha: Raanan family/AP Photo/picture alliance

Israel imethibitisha kuwa Hamas imewaachia huru mateka wawili iliokuwa inawashikilia, na tayari wamekabidhiwa kwa jeshi la Israel kwenye mpaka na Ukanda wa Gaza. Awali, Hamas ilisema katika tangazo lake kuwa mateka hao, mama na mwanaye wote raia wa Marekani, wameachiwa kwa sababu za kibinadamu chini ya upatanishi wa Katari.

Wakati huo huo jeshi la Israel limesema wengi kati ya mateka takribani 200 wanaoshikiliwa na Hamas wako hai, lakini halikufafanua zaidi juu ya chanzo cha taarifa hiyo. Vile vile Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel, ambayo yamejikita juu ya juhudi za kuachiwa huru kwa watu wanaoshikwa mateka, na kurahisisha upelekaji wa msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyetembelea kivuko cha Rafah kati ya Misri na Ukanda wa Gaza Ijumaa, kwa mara nyingine ametoa rai ya kutaka msaada uruhusiwe haraka katika Ukanda wa Gaza, akisema ni suala la maisha au kifo kwa wakaazi wa ukanda huo wapatao milioni 2.4.