1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg yaahidi kuikera Bayern

2 Novemba 2012

Hamburg SV yaapa kuikera tena Bayern Munich msimu huu wakati ligi ya Ujerumani Bundesliga ikirejea uwanjani baada ya michuano ya kombe la DFB Pokal,katikati ya wiki .

https://p.dw.com/p/16c1F
Fußball Bundesliga 6. Spieltag: Hamburger SV - Hannover 96 am 29.09.2012 in der Imtech Arena in Hamburg. Hamburgs Spieler jubeln mit dem Torschützen zum 1:0 Artjoms Rudnevs (l). Foto: Angelika Warmuth/dpa (Achtung Hinweis zur Bildnutzung! Die DFL erlaubt die Weiterverwertung von maximal 15 Fotos (keine Sequenzbilder und keine videoähnlichen Fotostrecken) während des Spiels (einschließlich Halbzeit) aus dem Stadion und/oder vom Spiel im Internet und in Online-Medien. Uneingeschränkt gestattet ist die Weiterleitung digitalisierter Aufnahmen bereits während des Spiels ausschließlich zur internen redaktionellen Bearbeitung (z. B. via Bilddatenbanken). +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kikosi cha timu ya Hamburger SVPicha: picture-alliance/dpa

Kocha wa Hamburg SV Thorsten Fink na mchezaji wa kati nyota wa timu hiyo Rafael van der Vaart wameahidi kuendeleza madhila yanayowakuta Bayern Munich kwa hivi sasa wakati watakapokuwa wenyeji wa vigogo hao wa soka la Ujerumani leo jioni.

GettyImages 152796194 MOENCHENGLADBACH, GERMANY - SEPTEMBER 26: Head coach Thorsten Fink of Hamburg looks on prior to the Bundesliga match between Borussia Moenchengladbach and Hamburger SV at Borussia Park Stadium on September 26, 2012 in Moenchengladbach, Germany. (Photo by Dennis Grombkowski/Bongarts/Getty Images)
Kocha wa timu ya Hamburger SV Thorsten FinkPicha: Getty Images

Viongozi wa ligi ya Bundesliga ,Bayern Munich walipigwa mwereka wa mabao 2-1 nyumbani kwao dhidi ya Bayer Leverkusen Jumapili iliyopita, kitendo kilichovunja mfululizo wa ushindi wa michezo nane katika Bundesliga msimu huu.

Hamburg , ikiwa katika nafasi ya saba, imekuwa katika hali nzuri ya mchezo hivi karibuni tangu pale mchezaji wa kiungo wa timu ya taifa ya Uholanzi Van der Vaart kurejea katika klabu hiyo mwezi August baada ya kukaa kwa muda Real Madrid na Tottenham Hotspurs.

Licha ya kuwa klabu hiyo iliyumba katika miaka ya hivi karibuni, Fink amebadilisha majaliwa yao kwa kupata saini ya Van der Vaart akiwa ni kiungo mchezeshaji akishirikiana na nyota kutoka Korea ya kusini Son Heung-Min, ambaye ni mfungaji mabao mengi katika klabu hiyo kwa sasa akiwa na mabao matano katika michezo tisa.

Hii ni timu tofauti kabisa ukilinganisha na msimu uliopita, amesema Fink wakati Hamburg ilipokuwa mkiani kabisa mwa msimamo wa ligi katika wakati kama huu.

Mabingwa watetezi Borussia Dortmund , ikiwa katika nafasi ya nne, wanamatumaini kuwa na nahodha wao Sebastian Kiel pamoja na mlinzi wa kati Mats Hummels watakuwa fit kwa ajili ya pambano la leo dhidi ya VFB Stuttgart. Kiel akipata maumivu ya mgongo na Hummels alicheza katika nusu moja tu ya mchezo wa kombe la shirikisho , DFB Pokal dhidi ya timu ya daraja la pili ya Aalen siku ya Jumanne, lakini kocha Jurgen Klopp amesema kuwa timu yake iko katika hali nzuri kuikabili Stuttgart.

Michezo mingine leo Jumamosi(03.11.2012) ni pamoja na Borussia Moenchengladbach ikiikaribisha Freiburg, Hannover 96 itakuwa wenyeji wa FC Augsburg, Nuremberg ikikabiliana na VFL Wolfsburg, Hoffenheim ikiangalia majaliwa yake dhidi ya Schalke 04 ambayo iko katika kiwango cha kutisha msimu huu na Hamburg ikiikaribisha Bayern Munich. Kesho Jumapili ni zamu ya Bayer Leverkusen ikionyeshana kazi na Fortuna Dusseldorf na Werder Bremen ina miadi na Mainz 05.

Chelsea yaonywa

Mchezaji wa ulinzi Gary Cahill ameionya Chelsea kutoruhusu msimu wao huu kuathiriwa na utata uliojitokeza nje ya uwanja katika klabu hiyo kabla ya mchezo wao na Swansea leo jioni.

Safari ya timu hiyo kuelekea Wales kupambana na Swansea imegubikwa na uamuzi wa Chelsea kutoa malalamiko yao rasmi dhidi ya mwamuzi Mark Clattenburg , wakidai mwamuzi huyo alitumia lugha mbaya dhidi ya mchezaji wa kiungo wa Chelsea John Obi Mikel wakati wa mchezo wa premier League dhidi ya Manchster United.

Chelsea's players stand together during a penalty shootout during their Champions League final soccer match against Bayern Munich at the Allianz Arena in Munich May 19, 2012. REUTERS/Kai Pfaffenbach (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER)
Kikosi cha FC ChelseaPicha: Reuters

Michezo mingine jioni ya leo(03.11.2012) katika Premier League ni kati ya Manchester United ikipambana na Arsenal, Fulham inaoneshana kazi na Everton, Manchester City iko ugenini dhidi ya West Ham United. Kesho Jumapili Liverpool inaikaribisha Newcastle United na Queens Park Rangers iko nyumbani ikiisubiri Reading.

Real yazinduka

Baada ya kuanza kwa kusua sua katika utetezi wa taji lake la La Liga nchini Uhispania ,Real Madrid imeweza sasa kubadilisha hali hiyo na licha ya kuwa inakabiliana na Barcelona ambayo inazidi kupaa , mlinzi Sergio Ramos anasema wataendelea kupambana na kufukuzana na mahasimu wao hao hadi mchezo wa mwisho.

Real Madrid's Cristiano Ronaldo from Portugal celebrates his goal during a Spanish La Liga soccer match against Levante at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, Spain, Sunday, Feb. 12, 2012. (Foto:Andres Kudacki/AP/dapd)
Mchezaji wa Real Madrid Cristiano RonaldoPicha: dapd

Michezo ya leo jioni(03.11.2012) ni kati ya Real Sociedad ikipambana na Espanyol, Deportivo la Coruna , inaonyeshana kazi na Mallorca, wakati Osasuna inapimana ubavu na Valladolid. Barca inaikaribisha Celta Vigo, wakati Real Madrid ina miadi na Zaragoza.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri:Moahammed Abdul-Rahman