1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANNOVER: Schroeder azindua kampeni ya uchaguzi

14 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEl7

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amezindua kampeni yake ya uchaguzi siku ya jumamosi.Schroeder amejaribu kuutumia ugomvi wa ndani wa chama cha upinzani cha kihafidhina CDU akitaraji kuimarisha nafasi ya chama chake cha SPD,ambacho hivi karibuni katika uchunguzi wa maoni kilionyesha kuwa na maendeleo fulani.Hata hivyo lakini chama SPD bado kinajikokota nyuma ya CDU.Na katika siasa ya kigeni,Kansela Schroeder kama ilivyokuwa wakati wa kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2002,kwa mara nyingine tena amejitenga na rais George W.Bush wa Marekani.Schroeder amepinga tishio la kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Iran.Ameuambia mkutano wa hadhara kuwa tishio la kutumia nguvu ni jambo lisiokubalika.Kansela Schroeder amependekeza kuwa na majadiliano imara pamoja na Iran.Miaka 3 ya nyuma wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu nchini Ujerumani,Schroeder alikataa kuishirikisha Ujerumani katika vita vya Iraq.Mwanasiasa wa chama cha upinzani cha CDU,Friedbert Pflüger anaeshughulikia masuala ya kigeni amesisitiza kuwa upande wa upinzani unaiunga mkono serikali kutafuta suluhisho la kidiplomasia kuhusu mzozo wa Iran.