Hannover. Ujerumani kuhifadhi data za simu na internet.
15 Machi 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Bwana Otto Schilly anania ya kuanzisha kituo cha kuhifadhi taarifa kwa ajili ya internet na simu katika juhudi za kupambana na ugaidi. Akizungumza katika eneo la maonesho ya vifaa vya compyuta mjini Hannover, Bwana Schilly amesema kuwa taarifa za mawasiliano zinapaswa kuhifadhiwa kwa muda wa hadi mwaka mmoja.
Hii imesema , itasaidia maafisa wa usalama kuweza kupata taarifa juu ya mipango ya mashambulizi ya magaidi.
Kwa hivi sasa , mawasiliano ya simu na internet nchini Ujerumani yanahifadhiwa kwa muda wa miezi mitatu.