HANOI: Mkutano wa APEC utafufua mazungumzo ya biashara duniani
19 Novemba 2006Matangazo
Mkutano wa kilele wa nchi za Asia-Pacifk-APEC umemalizika katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi.Katika taarifa ya kuufunga mkutano huo, viongozi wa nchi na serikali kutoka madola 21, wameahidi kufufua mazungumzo yanayojulikana kama „Duru ya Doha“ yakihusika na biashara duniani. Viongozi wa APEC,wameahidi kufanya kila wanachoweza ili kufufua mazungumzo hayo yaliokwama tangu mwezi wa Julai.Wakati huo huo wameamua kushirikiana kupiga vita ulaji rushwa. Ingawa viongozi hao walieleza wasi wasi wao kuhusu mradi wa kinuklia wa Korea ya Kaskazini,suala hilo halikutajwa katika taarifa ya pamoja ya kuufunga mkutano.