1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANOI: Mkutano wa APEC waagiza kuyafufua mazungumzo ya WTO yaliokwama

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCr7

Viongozi wa nchi 21 zinazounda jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi katika eneo la Asia na Pacifik-APEC waliokuwa katika mkutano wao mjini Hanoi nchini Vietnam, wamepania kutia msukumo mpya kwenye mazungumzo ya Shirika la biashara duniani, WTO, ambao yanazorota. Katika taarifa ya pamoja ya kukamilisha mkutano huo, viongozi hao wa APEC wameonya kuhusu madhara yanaoweza kutokea ikiwa mazungumzo ya mjini Doha yaliokwama mwezi Julai yatashindwa kabisa. Viongozi wa APEC wamekubaliana kufanya kila wawezalo kuyaokoa mazungumzo hayo. Wametoa pia taarifa ambamo wameelezea wasi wasi mkubwa kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea ya kaskazini. Kando na mkutano huo wa siku mbili, Marekani na Rushia zimesaini mkataba ambao umeifungulia njia Rushia kujiunga na Shirika la biashara duniani,WTO.

Rais wa Marekani, George W. Bush sasa yuko njiani kuelekea Indoneshia. Wakati rais Bush akielekea katika nchi hiyo yenye kuwa na idadi kubwa ya waislamu duniani, kumefanyika maandamano ya kuzipinga sera zake.