1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Morgan Tsvangirai apokea matibabu hospitalini

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJ9

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe,bwana Morgan Tsvangirai anapokea matibabu hospitalini baada ya kuachiwa huru pamoja na wanaharakati wengine wapatao darzeni kadhaa.Kiongozi huyo na wafuasi wengine wa upande wa upinzani walipigwa vibaya na polisi baada ya kukamatwa siku ya Jumapili.Tsvangirai anaekiongoza chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC,alipata majeraha mabaya kichwani na usoni alipokuwa mikononi mwa polisi. Leo asubuhi alitazamiwa kufika mahakamani lakini hali yake mbaya haikumruhusu kwenda kortini.Kwa mujibu wa mwanadiplomasia wa Kimarekani nchini Zimbabwe, hali ya kiongozi huyo wa upinzani ni “mbaya sana.”Wakati huo huo,Kamishna wa Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Louise Arbour ametoa wito wa kufanywa uchunguzi huru kuhusu madai ya kupigwa na polisi.