1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris afanya kampeni katika jimbo la Wisconsin

Josephat Charo
24 Julai 2024

Mgombea urais wa Marekani wa chama cha Democratic, makamu wa rais Kamala Harris, amefanya kampeni katika jimbo la Wisconsin, eneo la mapambano makali dhidi ya mpinzani wake Donald Trump wa chama cha Republican.

https://p.dw.com/p/4ieqH
Kamala Harris akiwa katika kampeni mjini Wisconsin
Mgombea urais wa Marekani wa chama cha Democratic, makamu wa rais Kamala HarrisPicha: Kamil Kraczynski/AFP

Mgombea urais wa Marekani wa chama cha Democratic, makamu wa rais Kamala Harris, amefanya kampeni katika jimbo la Wisconsin, eneo la mapambano makali dhidi ya mpinzani wake Donald Trump wa chama cha Republican.

Harris alishangiliwa na umati mkubwa wa watu na kutangaza kwamba uchaguzi wa Novemba 5 utakuwa chaguo kati ya uhuru na machafuko.

Harris aliwasili Milwaukee baada ya kupata uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wajumbe wa chama cha Democratic kuteuliwa rasmi kugombea urais kupitia tiketi ya chama hicho, baada ya rais Joe Biden kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.Kamala Harris aungwa mkono kugombea urais Marekani

Mkutano huo ulikuwa wake wa kwanza tangu alipoingia katika mbio za kuwania urais wa Marekani. Kwa upande mwingine Trump atafanya kampeni huko Charlotte, North Carolina, jimbo ambalo litakuwa eneo muhimu la mashindano makali katika uchaguzi wa Novemba.