1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris: Trump hataachwa kuwajibishwa ghasia za Capitol Hill

6 Septemba 2023

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amesema hii leo kwamba wale wote waliohusika na juhudi za kupindua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

https://p.dw.com/p/4W088
Kamala Harris
Makamu wa rais wa Marekani Kamala HarrisPicha: Misper Apawu/AP/picture alliance

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amesema hii leo kwamba wale wote waliohusika na juhudi za kupindua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 pamoja na vurugu katika jengo la bungewanatakiwa kuwajibishwa, hata kama atakuwa ni aliyekuwa rais Donald Trump.

Harris ameliambia shirika la habari la AP katika mahojiano huko Jakarta Indonesia kwamba, waache ushahidi na ukweli utamalaki, ili hatimaye hatua mahususi ziweze kuchukuliwa. Makamu huyo wa rais yuko Jakarta kuhudhuria mkutano wa kilele muungano wa Mataifa ya Kusini Mashariki wa Asia, ASEAN. 

Waendesha mashitaka wa shirikisho tayari wamemshitaki Trump kwa juhudi za kung'ang'ania madarakani na huko Georgia akishtakiwa kwa njama ya kupindua matakwa ya wapiga kura waliomchagua rais Joe Biden. 

Mapema leo, Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa kizalendo la Proud Boys Enrique Tarrio amehukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa jukumu lake katika shambulizi la jengo la bunge mnamo Januari 6 mwaka 2021.