Hatimaye Berlusconi ajiuzulu
13 Novemba 2011Matangazo
Berlusconi, mwenye umri wa miaka 75, alikuwa ameahidi kujiuzulu mara baada ya bunge kupitisha mpango wa kubana matumizi uliotakiwa na Umoja wa Ulaya. Bunge liliupitisha mpango huo kwa kura nyingi jana (12.11.2011) jioni, huku baraza la Senate likiwa limeshafanya hivyo tangu juzi.
Nafasi ya Berlusconi madarakani ilianza kuingia mashakani tangu Jumanne iliyopita, pale aliposhindwa kupata kura za kutosha bungeni. Mara tu habari za kujiuzulu kwa Berlusconi ziliposambaa, maelfu ya watu walikusanyika katikati ya mji mkuu, Rome, kushangiria kuondoka kwake. Nafasi yake inatazamiwa kuchukuliwa na kamishna wa zamani wa Umoja wa Ulaya, Mario Monti.
Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR
Mhariri: Sekione Kitojo