Ujumbe wa chama kikuu cha upinzani cha Tanzania, CHADEMA, uko kwenye ziara ya wiki mbili barani Ulaya, ukiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambapo pamoja na mengine unakutana na taasisi za kikanda na kimataifa kuzungumzia masuala ya demokrasia, haki za binaadamu na utawala bora yalivyo kwa sasa nchini mwake. Msikilize hapa akizungumza na Mohammed Khelef akiwa Brussels, Ubelgiji.