1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Havana. Kimbunga Dennis chaua watu 5 Haiti na 10 Cuba.

9 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvz

Kimbunga kikali kinachovuma katika eneo la visiwa vya karibiki kimesababisha vifo vya watu watano nchini Haiti na wengine 10 katika kisiwa cha Cuba.

Kimbinga hicho kinachojulikana kama Dennis kilishambulia maeneo ya kusini na kati ya Cuba jana Ijumaa, kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilometa 240 kwa saa.

Maafisa wa Cuba wamesema kiasi cha watu milioni 1.5 wamekimbia nyumba zao na wako katika maeneo ya muda ya kutoa misaada. Kituo kinachotumika na Marekani kuwaweka wafungwa nchini Cuba cha Guantanamo bay kinasemekana kuwa kimenusurika na kimbunga hicho.

Kimbunga hicho kilififia wakati kinaingia katika eneo la pwani ya kaskazini lakini kilipata kasi tena wakati kinaelekea katika maeneo ya Florida nchini Marekani.

Kinatarajiwa kutua katika maeneo kati ya jimbo la Florida na Lousiana nchini Marekani kesho Jumapili.