HAVANA: Wapinzani wakutana nchini Cuba
22 Mei 2005Matangazo
Makundi ya upinzani yamekutana nchini Cuba kwa mara ya mwanzo tangu takriban miaka 40.Serikali ya kikomunisti ya rais Fidel Castro haikuchukua hatua yo yote dhidi ya mkutano huo wa siku mbili uliofanywa katika nyumba binafsi karibu na mji mkuu Havana.Lakini serikali iliwazuia wanasiasa na waangalizi kadhaa kutoka Ulaya waliowasili Cuba kwa viza za utalii na walitaka kuhudhuria mkutano huo.Katika hati ya mwisho,wajumbe 150 wametoa muito wa kukomeshwa utawala wa chama kimoja nchini Cuba.Vile vile wametaka haki za binadamu ziheshimiwe na wafungwa wa kisiasa waachiliwe huru.