1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANNA:Mbunge wa Ujerumani atimuliwa Cuba

20 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFC4

Serikali ya Cuba imemtimua nchini humo mbunge wa ujerumani pamoja na senator mmoja wa jamhuri ya Czech .

Hatua hiyo imekuja muda mchache kabla ya watu hao kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na wapinzani wa serikali ya rais Fidel Castro wa Cuba.

Mwanadiplomasia mmoja wa Ujerumani amesema, Arnorld Vaatz,naibu mwenyekiti wa kundi la chama cha upinzani cha CDUCSU bungeni mjini Berlin aliwekwa ndani ya ndege na kurudishwa hapa Ujerumani.

Pamoja nae aliyetimuliwa ni Senator Karel Schwarzenberg wa jamhuri ya Czech na wabunge wawili wa bunge la ulaya kutoka nchini Poland wamekataliwa kuingia nchini humo.

Wote hao walikuwa miongoni mwa wabunge wa ulaya walioalikwa kuhudhuria mkutano mkuu wa mwanzo wa shirika linakusanya vikundi mbali mbali vya wapinzani wa Cuba.