Heiko Maas apinga vikwazo zaidi kwa Urusi
26 Aprili 2021Matangazo
Akizungumza na kituo cha utangazaji cha Ujerumani cha ARD, Maas ameuelezea uhusiano uliopo sasa kati ya Ujerumani na Urusi kuwa ni mbaya kabisa, lakini akisema hautakiwi kuendelea kuwa hivyo.
Amesema serikali ya Ujerumani inatakiwa kujihusisha zaidi na majadiliano na Urusi na kuongeza kuwa hicho ni kiini cha demokrasia.
soma zaidi: Zelensky, Macron, Merkel wazungumzia Ukraine mashariki
Katika hatua nyingine Maas amesema vikwazo vya Ujerumani dhidi ya Urusi kufuatia hatua yake ya kuinyakua Rasi ya Crimea vitaendelea hadi pale kutakapopatikana suluhu ya kisiasa.
Wakati huo huo, mahakama moja mjini Moscow imeyapiga marufuku mashirika yanayoongozwa na Navalny kuendesha shughuli zake.