1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HELSINKI: Mazungumzo ya WTO kufufuliwa ?

10 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDq

Mawaziri wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya wametoa mwito juu ya kuanzishwa tena mazungumzo ya biashara ya nchi wanachama wa shirika la biashara duniani WTO .

Mawaziri hao wametoa mwito huo kwenye mkutano wao uliofanyika mjini Helsinki ambapo wamesema kuwa kukwama kwa mazungumzo hayo kunaweza kuathiri ustawi wa uchumi duniani.

Mawaziri hao pia wameipongeza Ujerumani kwa juhudi ilizofanya katika kupunguza nakisi katika bajeti yake hadi kufikia asilimia 2 nukta 8 mwaka huu. Yaani chini ya asilimia 3 ,kiwango kinachokubalika kwa mujibu wa Mkataba uliotiwa saini na nchi zote za Umoja wa Ulaya.