1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah yadai kushambulia kwenye nyumba ya Netanyahu

22 Oktoba 2024

Kundi la Hezbollah limedai kuishambulia kwa droni nyumba ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wiki iliyopita na kukiri kwamba baadhi ya wapiganaji wake wamechukuliwa mateka na jeshi la Israel.

https://p.dw.com/p/4m6MG
Drone iliyoundwa Iran
Ndege isiyo na rubani iliyotengenezwa na Iran, inayoendeshwa na Hezbollah, ikiruka karibu na mpaka wa kusini wa Lebanon na kaskazini mwa Israel Novemba 11, 2023.Picha: AFP/Getty Images

Msemaji wa Hezbollah Mohammed Afif amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari kusini mwa Beirut, ambako jeshi la Israel liliwaagiza raia kuondoka. Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP amesema muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo Israel ililishambulia eneo hilo. Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken yuko nchini Israel katika ziara yake ya 11 tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, ambapo atakutana na Waziri Mkuu Netanyahu, kujaribu kufufua matumaini ya kusitishwa kwa vita huko mashariki ya kati.