1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hoeness aanza kutumikia kifungo chake jela

3 Juni 2014

Rais wa zamani wa Bayern Munich Uli Hoeness ameanza kutumikia kifungo kwa kukwepa kulipa kodi. Wakili wake amesema kuwa Hoeness ameripoti katika jela ya Landsberg am Lech kusini mwa Ujerumani

https://p.dw.com/p/1CAsS
Mitgliederversammlung des FC Bayern München Uli Hoeneß 2.5.2014
Picha: picture-alliance/dpa

Hoeness alihukumiwa na mahakama ya mjini Munich Machi mwaka huu kwa kukwepa kulipa kodi baada ya kuwa na akaunti ya siri nchini Uswisi na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu unusu.

Uli Hoeness alitangaza wazi kuwa ananuia kurejea katika klabu hiyo wakati alipotoa hotuba ya kuwaaga vigogo hao wa soka kabla ya kuanza kutumikia kifungo chake gerezani.

Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi ya ni vipi atakavyorejea, au katika kiwango au nyadhifa ipi baada ya kukamilisha kifungo chake cha miaka mitatu na nusu jela kwa mashitaka ya kukwepa kulipa kodi, lakini tangazo hilo lake lilishangiliwa katika mkutano wa kilele wa klabu hiyo, ambao makamu wake wa rais Karl Hopfner alichaguliwa kama mrithi wake.

Hoennes alikuwa rais wa Bayern Munich mwaka 2010, na mafanikio yaliendelea, kwa timu hiyo kushinda mataji matatu kwa msimu mmoja mwaka wa 2013. Herbert Hainer aliteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa baraza la ushauri la Bayern Munich.

Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman