1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hospitali kubwa zaidi ya Gaza inashindwa kutoa huduma

13 Novemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhima ya afya ya ulimwengu-WHO limesema hospitali kubwa zaidi katika eneo la Gaza, imeshindwa kutoa huduma na vifo miongoni mwa wagonjwa vikiongezeka.

https://p.dw.com/p/4YjuO
Nahostkonflikt - Schifa-Krankenhaus
Wagonjwa na hasa watu waliokimbia makazi yao wakuwa katika matibabu ndani ya hosptali ya Al-ShifaPicha: Khader Al Zanoun/AFP

Hospitali kadhaa katika eneo lililozingirwa la Palestina, ikiwemo ya al Shifa, zimezuiwa na vikosi vya Israel hatua imbayo pia inazua kutoa huduma za uangalizi wa kiafya kwa wale waliomo ndani. Na watoto watatu waliozaliwa wamekufa na kuna hatari kwa wagonjwa wengine kutokana na  hali ya kukatika kwa umeme. Kwa mujibu ya wanaohudumia hosptali hiyo wanasema karibu na kituo hicho cha afya kunaendelea mapigano makali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus ni kwamba ofisi yake ilifanikiwa kuzungumza na wataalamu wa afya katika hosptali hiyo, al-Shifa, ambao walielezea hali kuwa mbaya  na ya hatari na milio ya risasi na mabomu ya kila mara ikizidisha hali kuwa mbaya zaidi.

Kuna hofu ya vifo zaidi kuongezea ndani ya Hospitali ya al Shifa

Dokta Mohammed Qandil katika eneo la Gaza anaseama hali ni mbaya sana."Hali katika hospitali ya Al Shifa sasa ni mbaya sana. Haijawahi kutokea hali kama hii huko nyuma.Kuna ulengaji wa moja kwa moja wa majengo ya hospitali. Wenzetu walioko ndani katika hosptali hiyo wanakabiliwa na shida ya mawasiliano. Wanahisi kwamba wanakabiliwa na kifo bila msaada wowote au usaidizi.  Huu ni wito mwingine, wito wa mwisho, kwa watoa huduma za kiutu, tafadhali ongezeni shinikizo kuzuia mauaji haya dhidi ya walio katika hospitali. Alisema tabibu huyo.

Nahostkonflikt - Schifa-Krankenhaus
Watu wakiwa wamesimama nje ya kitengo cha kutoa huduma za dharura cha hosptali ya Al Shifa mjini Gaza.Picha: Khader Al Zanoun/AFP

Kwa operesheni hii ya sasa Israel inaendelea kwa kusema ipo katika jitihada za kuwakomboa mateza zaidi ya 200, ambao walichukuliwa na Hamas baada ya shambulizi la Oktoba 7 na kusema huduma za tiba zinapaswa kuhamishwa.

Takribani watu 180,000 wameandamana Ufaransa kupinga chuki dhidi ya Wayahudi

Nje ya eneo la Mashariki huko Ufaransa, jana Jumapili kumefanyika maandamano makubwa yaliojumuisha zaidi ya watu 180,000. Maandamano hayo ya kupinga kuongezeka kwa vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi, katika kipindi hiki cha vita vya Israel na Hamas ambayo yalijumuisha takribani watu 100,000 pekee kwa jiji la Paris, yalikusanya watu pia katika miji mingine.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Elisabeth Borne, wawakilishi wa vyama kadhaa vya mrengo wa kushoto, wahafidhina na wale wa mrengo wa kati wa Rais Emmanuel Macron pamoja na kiongozi wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen walihudhuria maandamano hayo. Rais Macron mwenyewe hakuhudhuria, lakini alionyesha kuunga mkono maandamano hayo na kutoa wito wananchi kusimama kidete dhidi ya kile alichokisema "kuzuka upya kusikoweza kuvumilika kwa watu wasiojizuilika kwa chuki dhidi ya Wayahudi."

Soma zaidi:Mashambulizi ya Israel yaendelea kutikisa Gaza

Hata hivyo, kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kushoto cha France Unbowed, Jean-Luc Melenchon, alijiweka kando ya maandamano, ambapo kabla, juma lililopita kupitia ukurasa wake wa  X zamani Twitter, akisema kwamba maandamano hayo yangekuwa mkutano wa kirafiki wa msaada usio na masharti kwa mauaji yanayoendelea huko Gaza.

Vyanzo: AP/RTR