1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Majeshi, wanamgambo wanaua raia Afrika Magharibi

17 Januari 2025

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema, makundi ya itikadi kali za Kiislamu na majeshi kote Afrika Magharibi yamekuwa yakiwauwa raia kiholela katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

https://p.dw.com/p/4pIfA
Burkina Faso
Wanajeshi wa Burkina FasoPicha: Kilaye Bationo/AP/dpa/picture alliance

Katika ripoti yake iliyotolewa Alhamisi, shirika hilo limeeleza kwamba Jeshi la Burkina Faso na wapiganaji wa kujitolea waliwaua raia wasiopungua 1,000 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2024. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika linalofuatilia mizozo la ACLED.

Soma: Washambuliaji wawaua wanajeshi karibu 15 wa Mali

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, vikosi vya usalama katika taifa jirani la Mali na washirika wao mamluki wa kundi la Wagner la Urusi vilihusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya raia katika sehemu ya operesheni zao zilizoyalenga makundi ya itikadi kali za Kiislamu na kusababisha vifo vya watu 1,021 kati ya Januari 1 hadi Oktoba 11.

Burkina Faso, Mali na Niger zimekuwa zikikabiliwa na mashambulizi ya makundi yenye uhusiano na kundi linalojiita dola la Kiislamu pamoja na Al Qaeda.