HRW: Mashambulizi yasababisha vifo vya watu wengi Tigray
11 Februari 2021Matangazo
Kulingana na ripoti ya shirika hilo vikosi vya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed vilizilenga nyumba za makaazi, hospitali, shule na masoko katika maeneo ya mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekele na miji mingine ya Shire na Humera. Human Rights Watch imeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza iwapo sheria za vita zilikiukwa kutokana na taarifa kwamba wanajeshi walifanya mshambulizi bila kubagua na kusababsiha vifo vya watu na kuharibu mali. Operesheni ya kijeshi dhidi ya jimbo la Tigray ilitangazwa Novemba mwaka uliopita na Waziri Mkuu Abiy aliyewatuhumu viongozi wa chama cha TPLF kilichokuwa kinaongoza eneo hilo kwa uhaini baada ya kuzishambulia kambi za jeshi la taifa.