Human Rights Watch yaituhumu Uturuki kuifungia Instagram
9 Agosti 2024Haya yanafanyika wakati shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch likisema, kufungwa kwa mtandao huo ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza.
Mamlaka pia imeufungia mchezo maarufu wa mtandaoni wa Roblox.
Human Rights Watch imetoa wito kwa serikali kuurudisha mtandao huo wa Instagram, ambao Rais Recep Tayyip Erdogan ameushtumu kwa kueneza ufashisti.
Mawaziri nchini humo pia wameushtumu mtandao wa Instagram kwa kushindwa kuzuia machapisho ambayo yametasfiriwa na mamlaka kama yenye maudhui yasiofaa.
Wiki iliyopita, mkurugenzi wa mawasiliano wa rais Erdogan, Fahrettin Altun, aliukosoa mtandao huo kwa kuzuia baadhi ya machapisho.
Mkurugenzi huyo aliikosoa Instagram kwa kuzuia watu kuchapisha ujumbe wa rambirambi kufuatia mauaji ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismael Haniyeh.
Erdogan, ambaye ni mshirika wa Haniyeh, alieleza mapema wiki hii kwamba mitandao ya kijamii haiwezi kile alichokiita "kuvumilia picha za mashahidi wa Kipalestina bila ya kuzipiga marufuku.”