1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW yasema waasi wa M23 huenda walihusika na mauaji Kishishe

14 Juni 2023

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda huenda walihusika na vifo vya watu waliozikwa kwenye makaburi ya pamoja katika kijiji cha Kishishe.

https://p.dw.com/p/4SZBd
Ukraine Krieg mit Russland | Gräber bei Izium
Picha: Hanna Sokolova/DW

Miili hiyo inaaminika kuwa ni ya wanavijiji na wanamgambo waliotekwa na baadae kuuliwa na waasi wa M23, kati ya Novemba 2022 na Aprili 2023, wakati kundi hilo lilipokuwa likiondoka Kishishe.

Human Rights Watch imerekodi visa vya mateso vilivyofanywa na waasi wa M23 katika eneo hilo la Kishishe baada ya kuzungumza na mashuhuda, kutizama picha za satelaiti, za kawaida na za video.

Soma zaidi: Waasi wa M23 wahusishwa na makaburi ya pamoja nchini DRC

Pamoja na visa hivyo vya mateso, waasi hao wa M23 walichoma moto nyumba moja iliyokuwa imefurika miili, kutumia shule tatu kama kambi zao, ingawa baadae walichoma moja ya shule hizo, hatua iliyowanyima watoto fursa ya kusoma.

Wakazi wa Kishishe walishuhudia mauaji ama mazishi ya miili hiyo wamesema kwamba makaburi ya pamoja yaliyorundikwa miili karibu 20 kwa kila kaburi yalichimbwa baada ya M23 kulidhibiti eneo hilo na baada ya kuondoka, baadhi ya makaburi ndipo yalipogunduliwa.