1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Hungary kupinga kujiunga kwa Bulgaria katika Schengen

16 Desemba 2023

Hungary imesema itapinga kujiunga kwa Bulgaria katika kanda ya uhuru wa kusafiri ya Umoja wa Ulaya, Schengen, ikiwa nchi hiyo haitandoa ushuru wa usafirishaji wa gesi ya Urusi

https://p.dw.com/p/4aFfW
Waziri wa mambo ya nje wa Hungary Peter Szijjarto wakati wa mkutano na wanahabari na mwenzake wa Cypruss  Ioannis Kasoulides  mnamo Oktoba 24, 2022
Waziri wa mambo ya nje wa Hungary Peter SzijjartoPicha: Danil Shamkin/NurPhoto/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, imemnukuu waziri wake Peter Szijjarto, akisema Hungary iliweka wazi kwa Bulgaria kwamba itapinga kujumuishwa kwake katika Schengen ikiwa ushuru huo dhidi ya njia yake kuu ya uagizaji wa gesi hautaondolewa.

Szijjarto ameongeza kuwa Hungary itabadilisha uamuzi wake punde tu ushuru huo utakapoondolewa.

Szijjarto asema hatua ya Bulgaria ilikiuka sheria

Szijjarto amesema hatua ya Bulgaria ambayo amesema ilienda kinyume cha sheria za Ulaya, ilitishia usalama wa usambazaji wa gesi hiyo sio tu kwa nchi hiyo lakini pia kwa Serbia na Macedonia Kaskazini.