1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Hungary yapuuza tetesi kuhusu Orban kuongoza baraza la Ulaya

9 Januari 2024

Tetesi hizo zimeibuka baada ya Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel kutangaza ghafla Jumapili kwamba atajiuzulu mapema ili asimame katika uchaguzi wa bunge la Ulaya utakaofanyika mwezi Juni.

https://p.dw.com/p/4b1Dw
Viktor Orban waziri mkuu wa Hungary
Viktor Orban waziri mkuu wa HungaryPicha: Omar Havana/AP/picture alliance

Hungary imetowa wito wa kupuuzwa tetesi kuhusu ikiwa Waziri Mkuu Viktor Orban aliyeingia kwenye mivutano mara chungunzima na Umoja wa Ulaya, huenda akaongoza kwa muda moja ya taasisi kubwa za Umoja huo.

Tetesi hizo zimeibuka baada ya Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel kutangaza ghafla Jumapili kwamba atajiuzulu mapema ili asimame katika uchaguzi wa bunge la Ulaya utakaofanyika mwezi Juni.

Hungary itachukuwa nafasi ya kupokezana ya mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya kuanzia mwezi Julai.

Na kwa sababu hiyo kwa mujibu wa sheria za sasa za Umoja huo ikiwa wanachama watashindwa kukubaliana kuhusu nani atarithi nafasi ya Michel, Orban ambaye ni mshirika wa Urusi huenda akaongoza kwa muda Baraza la Ulaya.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW