SiasaUholanzi
ICC yakabiliwa na shinikizo kufuatia waranti inazotoa
2 Desemba 2024Matangazo
Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, watazindua mkutano wao wa kila mwaka siku ya Jumatatu.
Wawakilishi wa nchi 124 wanachama wa ICC watajumuika mjini The Hague Uholanzi kuanzia Jumatatu hadi tarehe 7 katika mkutano wao wa 23 ambao wanatarajiwa kuichagua kamati mpya na kupitisha bajeti ya mahakama hiyo ya ICC.
ICC ilianzishwa mwaka 2002 na imekuwa kimbilio la mwisho la kuwafungulia mashitaka watu waliohusika na ukatili, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari.
Mahakama hiyo huanzisha kesi pale mataifa husika yasipokuwa na uwezo au kutoonyesha utayari wa kushtaki vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao.