ICC yasitisha uchunguzi machafuko baada ya uchaguzi Kenya
28 Novemba 2023Ofisi ya mwendesha mashataka wa Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu wa kivita.
ICC imetangaza kusimamisha uchunguziwake wa muda mrefu kuhusu machafuko yaliyosababisha umwagaji damu nchini Kenya yaliyozuka baada ya uchaguzi wa rais mwaka 2007.
Uamuzi huo waICC umetangazwa katika wakati ambapo ofisi ya mwendesha mashataka wake ikitoa mwito wa kuomba fedha za ziada kusimamia uchunguzi wa migogoro inayoendelea ikiwemo, Ukraine na vita vya Israel na Hamas.
Uchunguzi ulioanzishwa mwaka 2010 kuhusu machafuko ya Kenya, ulifanikisha hatua ya kufunguliwa mashtaka watuhumiwa sita wakiwemo rais wa sasa na wa zamani wa nchi hiyo.
Soma pia:ICC yaongeza juhudi za kufufua kesi dhidi ya Joseph Kony
Ingawa mahakama hiyo ilishindwa kuwatia hatiani kutokana na madai ya kutishwa kwa mashahidi pamoja na uingiliaji wa kisiasa.
Na baadae mashtaka yote dhidi ya watuhumiwa yalitupiliwa mbali.