ICJ yaitaka Israel kusitisha mashambulizi ya Rafah
24 Mei 2024Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo siku ya Ijumaa (24 Mei) ikieleza pia kuwa hali ya kibinaadamu ni mbaya.
Hata hivyo, ICJ imechelea kuamuru usitishaji kamili wa vita katika Ukanda wa Gaza.
Soma zaidi: Israel yadai kupata miili mitatu ya mateka Gaza
Akisoma uamuzi huo, Rais wa Mahakama hiyo, Nawaf Salam, alisema hatua za muda zilizoamriwa na mahakama mwezi Machi hazikushughulikia kikamilifu hali katika eneo hilo linalozingirwa kwa sasa.
Shauri hilo liliwasilishwa na Afrika Kusini kuitaka Israel isitishe mara moja operesheni yake ya kijeshi mjini Rafah.
Soma zaidi: Mahakama ya ICJ yatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu vita vya Gaza
Israel imekuwa ikipuuzilia mbali madai dhidi yake ya kufanya mauaji ya kimbari ikisema hayana msingi na kujitetea mahakamani kwamba operesheni yake katika Ukanda wa Gaza ni haki yake ya kujilinda dhidi ya wanamgambo wa Hamas walioishambulia mnamo Oktoba 7.