Idadi ya waliokufa katika shambulizi kambini Kongo yafika 35
10 Mei 2024Idadi ya watu waliokufa katikashambulizi la mnamo Mei 3 katika kambi ya wakimbizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imepanda na kufikia watu 35. Awali, maafisa wa kambi hiyo, walisema kwamba watu waliokufa walikuwa ni 15. Lakini taarifa iliyotolewa jana na waziri wa masuala ya jamii wa Kongo Modeste Mutinga Mutushayi ilisema watu waliouawa wamefikia 35 na wengine 37 wamejeruhiwa.
Mutushayi alitoa taarifa hiyo mjini Goma wakati alipotembelea kambi hiyo na kuambatana na ujumbe kutoka Kinshasa kutathmini shambulizi hilo. Marekani imeituhumu nchi jirani ya Rwanda na kundi la waasi la M23, inalosema linashirikiana na Kigali kuhusika na hujuma hiyo. Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya Marekani na kuyataja kuwa "kioja".
Soma pia: Marekani yataka Rwanda iwaadhibu askari kwa shambulizi Kongo
Kundi la M23 lilianzisha tena mashambulizi nchini Kongo mwaka 2021 na kudhibiti maeneo mengi.