1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Idadi ya waliuwawa kwenye mashambulizi ya Urusi yaongezeka

15 Juni 2023

Takriban watu sita wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mashambulizi mapya ya anga ya Urusi kwenye makazi ya watu huko Ukraine, huku mapigano makali yakiendelea katika maeneo ya kusini na mashariki.

https://p.dw.com/p/4SacE
Ukraine |  Odessa I shambulizi la drone la Urusi
Wafanyakazi wa zimamoto wakijaribu kuuzima moto katika jengo lililopigwa na shambulizi la drone la UrusiPicha: UKRAINIAN ARMED FORCES/REUTERS

Takriban watu sita wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mashambulizi mapya ya anga ya Urusi kwenye makazi ya watu huko Ukraine, huku mapigano makali yakiendelea katika maeneo ya kusini na mashariki wakati wapiganaji wa Ukraine wakijaribu kurejesha ardhi iliyonyakuliwa Urusi.

Mamlaka ya Ukraine jana Jumatano imesema watu watatu wameuwawa na wengine 13 wamejeruhiwa huko Odessa. Kadhalika katika mji wa Donetsk watu watatu waliuwawa na wengine sita walijeruhiwa.

Maafisa pia wanasema watu sita wamekufa baada ya kufyatuliwa mizinga na jeshi la Urusi awali Jumanne katika eneo la mpaka wa kaskazini-mashariki wa mkoa wa Sumy.

Katika makabiliano yanayondelea sasa serikali ya Ukraine inadai jeshi lake linawashambulia vikali la wanajeshi wa Urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na askari hao.