1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wanaojiunga na IS kutoka Balkan yarudi chini

31 Mei 2017

Wawakilishi wa Bosnia na Albania wanasema kwamba mtindo wa magaidi kutoka eneo la Balkan kujiunga na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, na makundi mengine ya itikadi kali nchini Syria na Iraq umepungua.

https://p.dw.com/p/2dsdH
Präsidentin Kosovo Atifete Jahjaga ARCHIV 2014
Rais wa Kosovo Atifete Jahjaga baada ya kumpokea kijana wa miaka 8 aliyepelekwa Syria na babakePicha: picture-alliance/AP Photo/V. Kryeziu

Taarifa hiyo ilitolewa katika mkutano wa hivi karibuni wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE. Makadirio ya idadi ya magaidi kutoka Balkan wanaojiunga na IS ni tofauti kuanzia wanamgambo elfu moja hadi maelfu, ingawa hakuna raia wa mataifa hayo aliyeondoka kuelekea Mashariki ya Kati katika miaka miwili iliyopita.

Panapoonekana dalili ndogo ya uwepo wa itikadi kali kwa usaidizi wa Dola la Kiislamu katika mataifa ya Balkan pasipo kujali huo ufanisi mdogo uliopatikana katika kupunguza wanaojiunga na kundi hilo, ni jambo linaloyaumisha kichwa mataifa makubwa ya magharibi.

Vedran Dzihic ni msomi na mtaalam wa eneo la Balkan katika taasisi ya Austria ya masuala ya kimataifa, "hakujakuwa na watu walioondoka kuelekea Syria na Iraq katika miaka miwili iliyopita Wasalafi, wapiganaji wa jihadi na Waislamu wenye itikadi kali walioko hapa miundo mbinu yao iko vile vile na sasa wameweka fahamu zao kwa nchi kadhaa na kanda nzima kwa ujumla," alisema Dzihic.

Dzihic anakadiria asilimia 30 hadi 40 ya wale walioondoka Kosovo au Bosnia na kuelekea Syria au Iraq, waliuwawa au walisalia huko. Karibu 150 wanakadiriwa kurudi Bosnia na chini ya 120 walirejea Kosovo.

Ushawishi wa Saudi Arabia ni tatizo 

Dzihic anasema na nikimnukuu, "tatizo la hawa wanaorejea bado lipo na bila shaka ni kitisho cha usalama," mwisho wa kunukuu. Serikali ya Marekani pia inalifahamu tatizo hilo. Naibu waziri Hoyt Yee hivi majuzi alikiambia kikao huko Washington D.C nchini Marekani kwamba bado kuna mengi yanayostahili kufanywa.

Scharmützel in Mazedonien
Mwanajeshi wa Macedoania akipambana na wapiganaji wa itikadi kali kutoka AlbaniaPicha: AP

"Wale waliopewa mafunzo ya itikadi kali wanaporudi nyumbani kutoka vitani, serikali za Balkan zina wasiwasi kwamba zitashuhudia ongezeko la machafuko, kukiukwa kwa sheria na itikadi kali katika eneo hilo, na labda jambo hilo lienee kaskazini na magharibi," alisema Yee mwezi Mei tarehe 17.

Siku hiyo hiyo wakati wa kikao cha bunge Berlin, bunge la Ujerumani lilisema kuongezaka kwa ushawishi wa Saudi Arabia na mataifa ya Ghuba ni tatizo lengine ambalo huenda likachangia ongezeko la mafunzo ya itikadi kali kwa Waislamu eneo la Balkan Magharibi.

"Mashirika la kimisionari ya Saudi Arabia yapo sana pia Kosovo ambapo yanaeneza tafsiri ya Wahhabi ya Uislamu kwa kutuma wahubiri," ilisema serikali ya Ujerumani kupitia taarifa.

Dzihic anasema hali ya masuala ya itikadi kali ilivyo sasa katika eneo la Balkan haitii wasiwasi lakini anaonya pia kwamba ishara lazima ziangaliwe kwa macho mawili.

Ukosefu wa kazi ni tatizo kubwa katika mataifa ya Balkan

"Ni kweli kwamba hali hii ipo, hali hii itasalia kuwepo na itayafuata maendeleo ya mataifa ya Balkan katika miaka na miongo kadhaa ijayo. Ni wazi pia kwamba Uislamu katika eneo la Balkan Magharibi hautakuwa hali sawa na jinsi ulivyokuwa katika miaka ya tisini."

Mtaalamu huyo anasema iwapo matatizo ya usalama, misukosuko na ugumu wa kiuchumi utaendelea, basi suala la itikadi kali pia litaongezeka.

Arabische TV-Serie "Black Crows" zum Ramadan
Wapaiganaji wa IS SyriaPicha: picture alliance/dpa/MBC group

Wasunni waliopewa mafunzo ya itikadi kali pamoja na matawi mengine ya itikadi kali katika Uislamu, yalijipenyeza kwa mara ya kwanza eneo la Balkan kupitia misikiti na wahubiri waliofadhiliwa na Saudi Arabia wakati wa vita vya Kosovo na Bosnia katika miaka ya tisini. Ushawishi wake umeenea pakubwa katika mwongo mmoja uliopita kutokana na hali ya kiuchumi na kijamii katika eneo hilo, na kwa ujumla ukosefu wa mwelekeo miongoni mwa vijana.

Mataifa sita ya eneo la Balkan ambayo ni Albania, Kosovo, Serbia, Macedonia, Bosnia na Montenegro yana tatizo kubwa la ukosefu wa kazi miongoni mwa vijana huku wengi walio na kazi wakipata mshahara unaokadiriwa kuwa euro 300 kwa mwezi.

Mataifa ya Balkan yaliyo na idadi kubwa ya Waislamu kama Kosovo, Albania na Bosnia na Herzegovina bado yanasemekana kuwa maeneo yanayokuza watu walio na misimamo mikali ya dini, ingawa majirani zao Macedonia, Serbia na Montenegro wanakabiliwa na tatizo hilo pia.

Mwandishi: Jacob Safari/DW

Mhariri: Josephat Charo