1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IEBC yakusanya masanduku ya kura

10 Agosti 2022

Maafisa wa tume ya IEBC wanaanza shughuli ya kusafirisha masanduku ya kupigia kura hadi kituo cha Taifa cha kujumlisha kura cha Bomas of Kenya.

https://p.dw.com/p/4FNKU
Kenia nach den Wahlen 2022
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Ili mshindi wa uchaguzi wa Rais atangazwe, sharti fomu asilia za 34A zifanyiwe uhakiki na tume yenyewe. Takwimu zinaashiria 64.5% ya wapiga kura wote walishiriki kwenye mchakato wa kuwasaka viongozi wapya. Kwa mujibu na tume ya uchaguzi ya Kenya,watu wasiopungua milioni 14 kati ya wote milioni 22 wenye sifa  walipiga kura kwenye uchaguzi wa Jumanne. 

Hata hivyo idadi hiyo haijajumlisha wapiga kura waliotambuliwa kutumia daftari asilia kwenye baadhi ya maeneo. Alasiri hii mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati alisisitiza kuwa sharti wapokee fomu zote za 34A zilizo na maelezo ya matokeo Kabla ya kumtangaza mshindi wa urais.

Tume ya uchaguzi ipo katika juhudi ya kusafirisha makasha ya kura.

Kwa sasa maafisa wa IEBC wako mbioni kusafirisha masanduku ya kupigia kura yenye matokeo yaliyo nakiliwa kwenye fomu 34A. Ifahamike kuwa tume ya uchaguzi ina wiki nzima ya kujumlisha na kuhakiki matokeo Kikatiba Kabla ya kumtangaza mshindi. Fomu hizo zinatokea vituo alfu 46 vya kuhesabia kura kote nchini.

Soma zaidi:Zioezi la kuhesabu kura za Wakenya linaendelea

Kwa upande ya uchaguzi Pwani ya Kenya, shirika moja la kiraia linawatolea wito viongozi wa kisiasa na wa Kenya kwa jumla kuvuta subra. Wajumbe wa Asasi hiyo ya Amani ya Taifa na Upatanishi, wanausisitizia umuhimu wa kuipa tume ya uchaguzi muda kufanya kazi yake bila Shinikizo ya kujumlisha na kuhakiki matokeo ya uchaguzi. Tarehe ya mwisho ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu ni ifikapo 16 Agosti.

DW: Nairobi