1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema Urusi yaimarisha ushirikiano wake na Iran.

10 Juni 2023

Ikulu ya White House imesema kuwa Urusi inaonekana kuimarisha ushirikiano wake wa ulinzi na Iran baada ya kupokea shehena ya ndege zisizokuwa na rubani kutoka Iran.

https://p.dw.com/p/4SPrV
USA | Capitol in Washington
Picha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Ikulu ya White House imesema kuwa Urusi inaonekana kuimarisha ushirikiano wake wa ulinzi na Iran baada ya kupokea shehena ya ndege zisizokuwa na rubani ambazo inazitumia kuishambulia Ukraine.

Ikinukuu nyaraka mpya za siri, Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa ndege hizo zilitengenezwa nchini Iran na kusafirishwa kupitia Bahari ya Caspian na sasa zinatumiwa na wanajeshi wa Urusi.

Msemaji wa Ikulu hiyo John Kirby amesema katika taarifa kuwa, Urusi inafanya kazi na Iran kuunda ndege zisizokuwa na rubani aina ya UAV ndani ya ardhi ya Urusi.

Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Marekani na Ukraine zinasema hatua ya Iran ya kuipa Urusi ndege zisizokuwa na rubani inakiuka makubaliano ya mwaka 2015 ya azimio la Baraza la usalama la Umoja wa mataifa juu ya mkataba wa nyuklia wa Iran.