Asili na mazingiraAzerbaijan
IMF na Benki ya Dunia kuendelea kushirikiana na Trump
13 Novemba 2024Matangazo
Wakuu hao aidha, wamesisitiza umuhimu wa kuzifadhili sekta binafsi kwenye nchi zinazoendelea zilizoathirika na mabadiliko ya tabianchi.
Mkuu wa Benki ya Dunia Kristalina Georgieva ameliambia jopo la watalaamu kwenye mkutano wa kimataifa wa mazingira, COP29 nchini Azerbaijan kwamba benki hiyo ilikwishafanya kazi na Trump huko nyuma na wataendelea kufanya hivyo.
Georgieva amesema pia kwamba ana imani kubwa sekta binafsi za Marekani zitaendelea kuwekeza katika teknolojia za kijani ili kuendeleza juhudi zilizokwishaanza.