SiasaPakistan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan azuiwa kugombea urais
31 Desemba 2023Matangazo
Tume ya Uchaguzi ya Pakistan, ECP ilimuengua Imran Khan baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi, lakini chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kiliwasilisha nyaraka zake za uteuzi wiki iliyopita kikipuuzia mbali hatua hiyo.
Msemaji wa (PTI), Raoof Hasan amesema asilimia 90 hadi 95 ya nyaraka za wagombea wao zimekataliwa.
Afisa mmoja wa tume ya uchaguzi amelithibitishia shirika la habari la AFP juu ya hatua hiyo, akisema imezingatia hatia dhidi ya wagombea hao ambao ni pamoja na Khan. Orodha ya wagombea wa mwisho itatangazwa Januari 23.
Khan amekuwa gerezani tangu mwezi Agosti akikabiliwa na msururu wa kesi ambazo anasisitiza zimechochewa ili kumzuia kuwania kwenye uchaguzi huo unaofanyika Februari 8, mwaka 2024.