Imran Khan na mkewe wahukumiwa miaka mingine 7 gerezani
3 Februari 2024Matangazo
Upande wa mashtaka ulisema Khan na mkewe walikiuka sheria inayosema mwanamke lazima asubiri miezi mitatu kabla ya kuolewa tena.Hukumu hiyo inafuatia kesi nyingine ya Jumatano iliyopita ambayo Khan na mkewe, Bushra Bibi, walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela kwa makosa ya rushwa.Hukumu hiyo inatolewa kabla ya uchaguzi wa wabunge wa Februari 8 ambao Khan tayari ameondolewa kwa sababu ya kukutwa kwake na hatia ya makosa ya ufisadi. Khan na familia yake wanasisitizakuwakesi hiyo imechochewa kisiasa. Hukumu hiyo ni ya nne kwa Khan, tangu alipoondolewa madarakani mwaka 2022.