1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

India na Ujerumani zakubaliana kuzalisha nishati safi

Saleh Mwanamilongo
26 Oktoba 2024

Ujerumani na India zimekubaliana kuanzisha utafiti na uzalishaji wa nishati safi ya hidrojeni. Hatua hiyo inaangazia juhudi zinazolenga kupatikana nishati mbadala.

https://p.dw.com/p/4mGkq
India na Ujerumani zakubaliana kuzalisha nishati mbadala ya hidrojeni
India na Ujerumani zakubaliana kuzalisha nishati mbadala ya hidrojeni Picha: Christian Bruna/Getty Images

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, amesema kuwa makubaliano hayo kuhusu hidrojeni hayamaanishi kuwa serikali zitafanya kila kitu ilikukamilisha mradi huo. Habeck amesema wanasayansi, wanafunzi na wafanyabiashara wa nchi mbili hizi lazima pia wajihusishe na mpango huo wa uzalishaji nishati mbadala.

Makubaliano hayop ya awali yanaelezea kwamba Ujerumani na India zinashiriki malengo ya pamoja ya kupunguza utegemezi wao juu ya uagizaji wa mafuta kutoka nje.