1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India yamfukuza balozi wa Canada

19 Septemba 2023

India imemfukuza mwanadiplomasia wa Canada na kuishutumu nchi hiyo kwa kuingilia masuala yake ya ndani, baada ya Ottawa kuituhumu New Delhi kwa mauaji ya mwanaharakati mmoja wa jamii ya Singasinga.

https://p.dw.com/p/4WXpJ
Kanada, BC, Surrey | Khalistan-Flaggen und ein Plakat sind vor dem Guru Nanak Sikh Gurdwara Sahib Tempel zu sehen
Picha: Chris Helgren/REUTERS

Uamuzi wa New Delhi umefanyika siku moja tu baada ya Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, kusema kuwa kulikuwa na madai ya kuaminika kwamba India ilikuwa inahusika na mauaji ya mwanaharakati Hardeep Singh Nijjar aliyeuawa Juni 18 nje ya kituo cha Utamaduni wa Singasinga kilichoko Surrey, British Columbia. 

Soma zaidi: OTAWA-Masingasinga wawili waachiwa huru kutokana na kesi ya uripuaji wa ndege ya abiria ya India mwaka 1985

India imekanusha madai hayo, ikisema ni ya kipuuzi. 

Canada nayo imemfukuza mwanadiplomasia wa India, huku mzozo wa mauaji hayo ukiongezeka.

Nijjar alikuwa akiandaa kura ya maoni isiyo rasmi kuhusu uhuru wa jamii ya Singasinga kutoka India. 

Mwanaharakati huyo alikuwa akitafutwa na maafisa wa India kwa madai ya kuhusika katika shambulizi linalodaiwa kumlenga kiongozi wa madhehebu ya Kihindu nchini India.